10 Wakaldayo wakamjibu mfalme: “Hakuna mtu yeyote duniani anayeweza kufanya jambo ambalo wewe mfalme unaagiza, kwa sababu hakuna mfalme yeyote mkuu wala gavana aliyewahi kumwomba kuhani yeyote mchawi, au mtu yeyote anayefanya mazingaombwe, au Mkaldayo afanye jambo kama hili.