-
Danieli 2:35Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
35 Wakati huo kile chuma, ule udongo wa mfinyanzi, ile shaba, ile fedha, na ile dhahabu, vyote pamoja, vikapondwapondwa na kuwa kama makapi kutoka kwenye uwanja wa kupuria wakati wa kiangazi, kisha upepo ukavipeperusha mbali hivi kwamba hakuna chembe yoyote ya vitu hivyo ingeweza kupatikana. Lakini lile jiwe lililoipiga ile sanamu likawa mlima mkubwa, nalo likaijaza dunia yote.
-