3 Basi maliwali, wasimamizi, magavana, washauri, watunza-hazina, waamuzi, mahakimu, na wakuu wote wa mikoa wakakusanyika kwa ajili ya sherehe ya kuzindua sanamu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa amesimamisha. Nao wakasimama mbele ya sanamu iliyosimamishwa na Nebukadneza.