12 Majani yake yalipendeza, na matunda yake yalikuwa mengi, nao ulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Wanyama wa mwituni walitafuta kivuli chini yake, na ndege wa angani walikaa kwenye matawi yake, na viumbe wote walipata chakula kutoka katika mti huo.