4 Wakati huo maofisa wakuu na maliwali walikuwa wakitafuta msingi fulani wa kumshtaki Danieli kuhusiana na mambo ya serikali, lakini hawakuweza kupata msingi wowote wa kumshtaki wala ufisadi wowote, kwa sababu alikuwa mwenye kutegemeka, naye hakupatikana kamwe akiwa mzembe wala mfisadi.