17 Naye ataazimia kabisa kuja na nguvu kamili za ufalme wake, atafanya makubaliano pamoja na mfalme huyo; naye atatenda kwa mafanikio. Na kumhusu yule binti wa wanawake, mfalme huyo atapewa ruhusa ya kumwangamiza. Na binti huyo hatasimama, wala hataendelea kuwa wake.