3 Kwa hiyo Abrahamu akaamka asubuhi na mapema na kumtandika punda wake, akachukua wawili kati ya watumishi wake na Isaka mwana wake;+ naye akapasua kuni kwa ajili ya toleo la kuteketezwa. Kisha akaondoka, akafunga safari kwenda mahali ambapo Mungu wa kweli alimwonyesha.