30 Ikawa kwamba alipoona ile pete ya puani na vikuku+ mikononi mwa dada yake na aliposikia maneno ya Rebeka dada yake, akisema: “Hivi ndivyo huyo mwanamume alivyosema nami,” ndipo akaja kwa huyo mwanamume na tazama alikuwa hapo, amesimama kando ya ngamia kwenye chemchemi.