Maelezo ya Chini
a Kwa hakika, uchunguzi wa karibuni umeonyesha kwamba hata vijana walio katika miaka yao ya 20 huugua kwa kadiri kubwa wakati wazazi wao wanapotalikiana. Ule mgeuzo wa wazi wa adili za wazazi wao huwaacha wakiwa wameduwaa, yaripoti The New York Times Magazine. Wengi huangukia kwenye anasa na ukosefu wa adili, hali wengine hujiepusha na mahusiano yoyote yale ya kimahaba, wengine wakiapa kwamba hawataoa kamwe.