Maelezo ya Chini
a Mwanahistoria Myahudi wa karne ya kwanza Joseph ben Matthias (Flavio Yosefu) aandika kwamba kufikia wakati huo, makuhani wakuu wa Israeli waliwekwa na kuondolewa na mawakili wa Roma kadiri ya mara moja kila mwaka. Katika hali hiyo, ukuhani wa juu uligeuka ukawa cheo cha kukodiwa kilichovutia watu wabaya zaidi katika jamii. The Babylonian Talmud hutaja maadili ya kupita kiasi ya baadhi ya makuhani hao wakuu. (Pesaḥim 57a) Ile Talmudi pia hutaja nia ya Mafarisayo kuelekea unafiki. (Soṭah 22b)