Maelezo ya Chini
b Bila shaka, ni lazima wazazi wawaoshe na kuwabadili mavazi watoto wadogo sana, na katika nyakati hizo wazazi huosha viungo vya faragha. Lakini wafunze watoto wako waoge wenyewe mapema; wastadi fulani wa utunzaji wa watoto hupendekeza kwamba wajifunze kuosha viungo vyao vya uzazi wakifikia umri wa miaka mitatu ikiwezekana.