Maelezo ya Chini
a Petro, Yakobo, na Yohana walishuhudia mgeuko-sura wa Yesu (Marko 9:2) na ufufuo wa binti ya Yairo (Marko 5:22-24, 35-42); walikuwa karibu na Bustani la Gethsemane wakati wa jaribio la kibinafsi la Yesu (Marko 14:32-42); na wao, pamoja na Andrea, walimwuliza Yesu kuhusu uharibifu wa Yerusalemu, kuwapo kwake kwa wakati ujao, na umalizio wa mfumo wa mambo.—Mathayo 24:3; Marko 13:1-3.