Maelezo ya Chini
d Uchunguzi wa karibuni wadokeza kwamba mchanganyiko wa lishe ya maziwa na unyonyeshaji huenda ukaongeza hatari ya maambukizo ya HIV na kwamba maziwa ya mama huenda yakawa na vizuia-virusi ambavyo husaidia kuzimua virusi. Ikiwa ni kweli, kunyonyesha peke yake—hata kukiwa na hatari zake—kwaweza kuwa chaguo salama zaidi. Hata hivyo, utafiti wa uchunguzi huo haujathibitishwa bado.