Maelezo ya Chini
a Alama g inatumiwa katika kukadiria kiasi cha kani zinazoathiri watu wakiwa ndani ya aina yoyote ya chombo cha usafiri. Nguvu ya uvutano ya dunia hutokeza mchapuko wa wastani wa 1 g. Wakati ambapo rubani anaelekeza ndege juu, yeye huhisi kani ya ziada ikimsukuma kwenye kiti chake. Iwapo kani hiyo ni mara mbili ya nguvu ya uvutano, basi inapewa alama ya 2 g.