Maelezo ya Chini
a Iwapo blanketi ya kuzima moto hutumika kwa ukawaida katika nchi yenu, basi hakikisha unajua jinsi ya kuitumia ifaavyo. Shirika la Kujikinga na Moto la Kitaifa la Marekani lasema hivi: “Inapasa kukaziwa kwamba . . . blanketi ya kuzima moto si muhimu sana. Zapasa kutumiwa tu iwapo zapatikana kwa urahisi. . . . Kutumia blanketi ya kuzima moto isivyofaa kwaweza kuzidisha majeraha ya moshi na moto iwapo blanketi yapeperusha moshi kuelekea uso au ikiwa blanketi haiondolewi mara moto uzimikapo.”