Maelezo ya Chini
a Msukumo wa damu hupimwa kwa kimo, katika milimeta, ambacho msukumo huo huinua kiasi mahususi cha hidrajiri. Msukumo wa juu na wa chini unaosababishwa na mpigo na mkunyato wa moyo huitwa msukumo wa damu wakati wa mkunyato (systolic pressure) na kutunuka kwa moyo (diastolic pressure). Msukumo huo hubadilika kulingana na umri wa mtu, jinsia, mkazo wa kiakili na kimwili, na uchovu. Wanawake huelekea kuwa na msukumo wa chini wa damu kuliko wanaume, watoto huwa na msukumo wa chini na wazee huwa na msukumo wa juu zaidi. Ingawa huenda maoni yakatofautiana kidogo, kijana mwenye afya anaweza kuwa na kipimo cha milimeta 100 hadi 140 cha systolic ya hidrajiri, na milimeta 60 hadi 90 za diastolic.