Maelezo ya Chini
b Shirika la AIM ni shirika linalotetea haki za raia lililoanzishwa na Mhindi mmoja Mwekundu katika mwaka wa 1968. Mara nyingi shirika hilo huchambua shirika la BIA, ambalo ni shirika la serikali lililoanzishwa mwaka wa 1824, eti kwa madhumuni ya kuendeleza masilahi ya Wahindi Wekundu nchini. Mara nyingi shirika la BIA liliwauzia watu wasio Wahindi Wekundu haki za kutumia madini, maji na haki nyinginezo kwenye makao ya Wahindi Wekundu.—World Book Encyclopedia.