Maelezo ya Chini
a Jaribio fulani sahili linaonyesha kwamba kuna shinikizo la hewa. Ukikwea mlimani na chupa tupu ya plastiki, kisha uijaze hewa na kuifunika kabisa, ni nini kitakachotokea unaposhuka mlima huo? Chupa hiyo itabonyea. Shinikizo la hewa nje ya chupa linazidi sana shinikizo la hewa nyepesi iliyo ndani ya chupa.