Maelezo ya Chini
a Msomaji yeyote mwenye kufuata haki atakubali kwamba kusema jua limesimama angani kunamaanisha kwamba hivyo ndivyo mtu anavyoliona, wala si mchanganuo wa kisayansi. Hata wataalamu wa mambo ya angani mara nyingi husema kwamba jua, sayari, na nyota huchomoza na kutua. Huwa hawamaanishi kwamba magimba hayo ya mbinguni huzunguka dunia, lakini, badala yake, hayo huonekana kana kwamba yanasonga angani.