Maelezo ya Chini
a Maelfu ya korongo kutoka Asia na Ulaya hupita nchi ya Israel wanapohama kabla ya majira ya baridi kali kuanza katika maeneo yao ya kuzalia na wanaporudi kwenye maeneo hayo. Wengine wao pia huhamia nchi hiyo. Jioni-jioni katika sehemu ya kaskazini ya Bonde la Yordani, watu wanaweza kuona vikundi vya korongo wakipita Mlima Hermoni uliofunikwa kwa theluji. Lakini mandhari hiyo yenye kuvutia huonekana kwa muda mfupi tu.