Maelezo ya Chini
a Maneno bitumeni, lami ya asphalt, na bereu hutumiwa mara nyingi kumaanisha kitu kilekile. Hata hivyo, bitumeni ni mchanganyiko mweusi wa kemikali ya kaboni na hidrojeni ulio katika lami, bereu, na petroli. Lami nayo ni mchanganyiko mweusi unaonata ambao hubaki wakati mbao, makaa ya mawe, na mboji zinapochomwa kwa moto. Lami inapovukizwa zaidi hutokeza mchanganyiko mzito unaoitwa bereu. Lami na bereu zina kiasi kidogo cha bitumeni.
Petroli, au mafuta yasiyosafishwa, yanapovukizwa hutokeza mchanganyiko ulio na bitumeni nyingi. Bitumeni inayotokana na petroli huitwa pia lami ya asphalt. Hata hivyo, katika sehemu nyingi “lami” hiyo huonwa kuwa mchanganyiko wa bitumeni na vitu kama mchanga au changarawe, ambao hasa hutandazwa barabarani. Katika makala hii, neno lami limetumiwa kumaanisha “lami ya asphalt” isiyosafishwa au iliyosafishwa kutoka kwenye Ziwa la Lami.