Maelezo ya Chini
a Kwa nini jiji hilo linaitwa “D.C.” (District of Columbia)? Linaitwa hivyo kwa sababu halimilikiwi na jimbo lolote kwani liko katika ardhi ya serikali yenye ukubwa wa kilometa 177 za mraba. Pia jina “D.C.” hulitofautisha na jimbo la Washington, lililo kwenye Pwani ya Magharibi, kilometa 3,000 hivi kutoka katika jiji hilo.