Maelezo ya Chini
a Kindi huyo ni mmoja kati ya zaidi ya aina 30 za kindi wanaoruka. Wengi wao kutia ndani kindi wanaoruka ambao wanatoshana na paka huishi katika misitu ya Kusini-Mashariki mwa Asia. Kwa kawaida, kindi wanaoishi Afrika hawaorodheshwi kati ya virukanjia ingawa wanafanana sana. Sehemu pekee inayowatambulisha ni mkia wao ambao una manyoya kwenye ncha tu na sehemu ya chini.