Maelezo ya Chini
a Merengue ni aina fulani ya muziki wa dansi. Zamani, kikundi kidogo cha wanamuziki kilicheza merengue kwa kutumia kodiani, guiro (kikwanguzi cha chuma), na tambora (ngoma mbili ndogo zilizounganishwa). Baada ya muda, bendi kubwa zaidi (ambazo pia ziliitwa okestra katika Jamhuri ya Dominika) zilianzishwa. Kwa sasa, vikundi vingi vya merengue hutumia piano, saksafoni, tarumbeta, na ngoma za conga, na pia ala nyingine.