Maelezo ya Chini
d Kwa kawaida, karibu gramu saba za kileo huondolewa mwilini kila baada ya saa moja. Kila nchi ina kiwango chake cha kipimo cha kawaida. Shirika la Afya Ulimwenguni linafafanua kipimo cha kawaida kuwa gramu 10 za ethanoli. Kiasi hicho ni sawa na mililita 250 za bia, mililita 100 za divai, au mililita 30 za kileo kikali.