Maelezo ya Chini
a Neno “mumiani” linatokana na neno la Kiarabu mummiya, linalomaanisha “lami” au “bereu.” Hapo awali neno hilo lilitumiwa kwa maiti iliyopakwa utomvu kwa sababu ya weusi wake. Sasa neno hilo hutumiwa kurejelea mwili wowote ule uliohifadhiwa, wa mwanadamu au wa mnyama hata kama umehifadhiwa kiaksidenti au kwa kusudi fulani.