Maelezo ya Chini
a Ni hatari kuwagusa ndege waliojeruhiwa, kwa sababu hawajui kwamba unataka kuwasaidia. Pia, ndege fulani wanaweza kuwaambukiza wanadamu magonjwa. Kwa hiyo, ikiwa unataka kumsaidia ndege aliyejeruhiwa, vaa glavu na unawe mikono baadaye. Ikiwa unahofia afya au usalama wako, usimkaribie ndege huyo. Ikitegemea hali, unaweza kuomba msaada wa wataalamu.