Maelezo ya Chini
a Kufanya mazoezi kupita kiasi hivi kwamba wanawake wanakosa hedhi kunaweza kudhoofisha mifupa kwa kukosa estrojeni. Inapendekezwa kwamba wanawake walio na umri unaozidi miaka 65 wapimwe uzito wa mifupa yao ili ionekane mifupa imedhoofika kwa kiasi gani. Ikiwa imedhoofika sana, kuna dawa zinazoweza kuzuia na kutibu ugonjwa huu wa mifupa. Hata hivyo, mtu anapaswa kufikiria hatari na faida kabla ya kuanza matibabu hayo.