Maelezo ya Chini
a Baada ya utawala wa Mfalme Sulemani, taifa la Israeli lenye makabila 12 liligawanyika. Makabila ya Yuda na Benyamini yalifanyiza ufalme wa kusini; na yale makabila mengine kumi yakafanyiza ufalme wa kaskazini. Yerusalemu ulikuwa mji mkuu wa ufalme wa kusini, na Samaria ukawa mji mkuu wa ufalme wa kaskazini.