Maelezo ya Chini
b Wataalamu wa nyota wa Ugiriki walianzisha utaratibu wa kupiga hesabu ili kujua thamani ya pembe na pande za pembetatu. Wasomi Waislamu walitumia hesabu za pembe au trigonometria kujua upande wa Mecca. Waislamu wanapenda kusali wakitazama upande wa Mecca. Pia, hufuata utaratibu wao kwa kuchimba makaburi na kuzika wafu kuelekea upande wa Mecca na wauzaji wa nyama ambao ni waumini wa dini ya Kiislamu, hupenda kuangalia upande wa Mecca wanapochinja wanyama.