Maelezo ya Chini
a Nyakati nyingine, afya ya mama au mtoto inaweza kuwa hatarini, lakini hiyo haipaswi kuwa sababu ya kutoa mimba. Ikitokea kwamba wakati wa kujifungua hali inalazimu mmoja kati ya mama au mtoto apoteze uhai, ni jukumu la wenzi wa ndoa kuamua. Lakini maendeleo ya tiba katika nchi zilizoendelea yamefanya visa vya aina hiyo viwe vichache sana.