Maelezo ya Chini
c Cyclopedia ya McClintock na Strong (Buku la 10, uku. 519) huripoti: “Wamaliki walilazimishwa wauone Ukristo na ghasia zilizochochewa miongoni mwa raia na makuhani wapagani ambao walitazama kwa hofu maendeleo yenye kustaajabisha ya imani hiyo, naye Trajani [98-117 W.K.] kwa sababu hiyo aliongozwa atoe amri za kukandamiza polepole hilo fundisho jipya lililogeuza watu kuwa wachukiaji wa tumungu. Usimamizi wa Plini mchanga akiwa gavana wa Bithinia [iliyopakana na mkoa wa Kiroma wa Esia upande wa kaskazini] ulitatizwa na mambo yaliyotokana na mweneo wa haraka sana wa Ukristo na hasira kali ya raia wa kipagani ndani ya jimbo lake.”