Maelezo ya Chini
c Ingawa tafsiri nyingi hufasiri fungu hili la maneno “kushinda” (Swahili Union Version, Revised Standard, The New English Bible, King James Version) “akiwa amenuia kupata ushindi” (Phillips, New International Version), tumizi hapa la namna ya kitenzi katika Kigiriki asilia bila kuonyesha kukamilika au muda wa tendo hutoa maana ya ukamilisho au mwisho kabisa. Kwa sababu hiyo, Word Pictures in the New Testament cha Roberts hutoa elezo hili: “Kitenzi-wakati hapa cha kutoonyesha kukamilika au muda wa tendo huelekeza kwenye ushindi wa mwisho kabisa.”