Maelezo ya Chini
b Ingawa nyota saba katika mkono wa kulia wa Yesu ni picha ya waangalizi waliopakwa mafuta katika kundi la Kikristo, walio wazee katika makundi 100,000 hivi katika ulimwengu leo ni wale wa umati mkubwa. (Ufunuo 1:16; 7:9) Cheo chao ni nini? Kwa kuwa wao hupokea kuwekwa kwao kwa njia ya roho takatifu kupitia jamii iliyopakwa mafuta ya mtumwa mwaminifu na mwenye uangalifu, hawa wanaweza kusemwa kuwa wako chini ya mkono wa kulia wenye udhibiti wa Yesu kwani wao pia ni wachungaji walio chini yake. (Isaya 61:5, 6; Matendo 20:28) Wao huunga mkono “nyota saba” katika maana ya kwamba wao hutumikia mahali ambako ndugu waliopakwa mafuta wenye kustahili hawapatikani.