Maelezo ya Chini
a Akionyesha chanzo kisicho cha Kikristo cha mengi ya mafundisho, sherehe, na mazoea ya Jumuiya ya Wakristo iliyoasi imani, John Henry Newman kardinali Mkatoliki wa karne ya 19 aliandika hivi katika kichapo chake Essay on the Development of Christian Doctrine: “Utumizi wa mahekalu, na hayo yakiwa yamewekwa wakfu kwa watakatifu fulani, na pindi nyingine yakiwa yametiwa madoido ya matawi ya miti; uvumba, mataa, na mishumaa; matoleo ya kushuhudia wakfu baada ya kupata nafuu ya ugonjwa; maji matakatifu; nyumba za kutunzia mayatima na wenye shida; sikukuu na misimu, tumizi la kalenda, miandamano, kubarikia mashamba; mavazi ya makasisi, kipara utosini, pete katika ndoa, kugeukia Mashariki, mifano kwenye tarehe ya baadaye, labda wimbo wa kieklesia, na Kyrie Eleison [wimbo “Bwana, Urehemu”], chanzo cha yote ni upagani, yakatakaswa kwa kukubaliwa ndani ya Kanisa.”
Badala ya kutakasa ibada ya sanamu kama hiyo, “Yehova Mweza Yote” huonya Wakristo “Ondokeni kutoka miongoni mwao, na kujitenga nyinyi wenyewe, . . . na acheni kabisa kugusa kitu kisicho safi.”—2 Wakorintho 6:14-18, NW.