Maelezo ya Chini
d Kwa kupendeza, sanamu moja ya mtawala fulani wa kale iliyopatikana kaskazini mwa Siria katika miaka ya 1970 ilionyesha kwamba ilikuwa kawaida kwa mtawala kuitwa mfalme wakati, kihalisi, alikuwa na cheo cha chini zaidi. Sanamu hiyo ilikuwa ya mtawala wa Gozani na ilichorwa katika Kiashuri na Kiaramu. Mchoro wa Kiashuri ulimwita mwanamume huyo liwali (gavana) wa Gozani, lakini mchoro uliolingana na huo wa Kiaramu ulimwita mfalme.9 Kwa hiyo haingekuwa mara ya kwanza Belshaza kuitwa mwana-mfalme mteuliwa katika michoro rasmi ya Kibabuloni ambapo katika mwandiko wa Kiaramu wa Danieli anaitwa mfalme.