Maelezo ya Chini
a Miongoni mwa sosaiti za Biblia nyingi zilizofanyizwa tangu 1804 ni Sosaiti ya Biblia ya Amerika (1816), iliyoundwa kutokana na sosaiti za huko ambazo tayari zilikuwa zimekuwako, na pia Sosaiti ya Biblia ya Edinburgh (1809) na Sosaiti ya Biblia ya Glasgow (1812), zote mbili ziliunganishwa kuwa shirika moja (1861) katika Sosaiti ya Biblia ya Kitaifa ya Scotland. Kufikia 1820 sosaiti za Biblia zilikuwa zimeundwa pia katika Switzerland, Ireland, Ufaransa, Finland, Sweden, Denmark, Norway, Uholanzi, Iceland, Urusi, na Ujerumani.