Maelezo ya Chini
a Simulizi katika kitabu cha Mwanzo lielezalo bustani ya Edeni si fumbo la maneno, bali Edeni palikuwa mahali hasa palipokuwa pakubwa. Andiko hilo huelekeza kwenye mahali kaskazini mwa nyanda za Mesopotamia, chanzo cha mito Frati na Tigri. (Mwanzo 2:7-14) Ilipaswa kutumika kuwa kiolezo, ambacho kulingana nacho mtu angefananisha na kulima sehemu nyingine ya dunia.