Maelezo ya Chini
b Tokea wakati wa utawala wa Aleksanda Mkuu (336-323 K.W.K.), Wagiriki walitia jitihada kubwa kueneza falsafa, utamaduni, na lugha yao kwenye nchi zote zilizotiwa ndani ya Milki ya Ugiriki. Wale waliokubali utamaduni na kufikiri kwa Kigiriki walionwa kuwa wamegeuzwa kuwa Wagiriki. Jitihada hiyo ya kushinda tamaduni nyinginezo na kuziingiza katika ule wa Ugiriki uliendelezwa chini ya Milki ya Roma, ambayo, ijapokuwa ilikuwa imeshinda Ugiriki, ilipata utamaduni na falsafa zake kuwa zenye kuvutia. Hata miongoni mwa wengi kati ya wale waliopinga kwa bidii yenye kuendelea wimbi hilo kubwa la uvutano wa Kigiriki, twapata uthibitisho ulio wazi kwamba walikubali mawazo, hoja, na mafundisho ya kifalsafa ya Kigiriki.