Maelezo ya Chini
a Baadhi ya watu hudai kwamba maandishi hayo hujipinga yenyewe au kwamba hupinga Maandiko ya Kiebrania. Hata hivyo, uchunguzi wa hayo yanayodhaniwa kuwa mapingano huthibitisha kwamba sivyo ilivyo. Kwa kweli, kanuni ile ile iliyotumika kwa yanayodhaniwa kuwa mapingano ndani ya Maandiko ya Kiebrania yenyewe yatumika hapa. (Ona sehemu ya “Biblia—Je! Imepuliziwa na Mungu?,” mafungu 9 hadi 12.) Kwa kuwa Wakristo wote wa kwanza, kutia na wale walioandika vitabu vilivyojumuika kuwa Maandiko ya Kigiriki ya Kikristo, walikuwa Wayahudi, hawakuchochea upinzani dhidi ya Wayahudi kama wasivyofanya wale manabii Wayahudi kabla yao ambao walishutumu viongozi wa kidini wa siku zao.