Maelezo ya Chini
b Washiriki watano wa Halmashauri ya Uhariri kama vile walivyotajwa katika wasia wa Russell walikuwa William E. Page, William E. Van Amburgh, Henry Clay Rockwell, E. W. Brenneisen, na F. H. Robison. Kuongezea, ili kujaza nafasi zozote zilizoachwa wazi, wengine walitajwa—A. E. Burgess, Robert Hirsh, Isaac Hoskins, G. H. Fisher, J. F. Rutherford, na John Edgar. Hata hivyo, Page na Brenneisen walijiuzulu mara moja—Page kwa sababu hangeweza kuhama na kuishi Brooklyn, na Brenneisen (baadaye mwendelezo ulibadilishwa kuwa Brenisen) kwa sababu alilazimika kufanya kazi ya kimwili kuruzuku familia yake. Rutherford na Hirsh, ambao majina yao yalikuwa yameorodheshwa katika The Watch Tower la Desemba 1, 1916, walichukua mahali pao wakiwa washiriki wa Halmashauri ya Uhariri.