Maelezo ya Chini
c Kulingana na katiba ya Watch Tower Society, baraza la waelekezi lilipasa kuwa na washiriki saba. Katiba hiyo iliandaa nafasi ili washiriki walio hai wa baraza la waelekezi wajazie nafasi iliyo wazi. Hivyo, siku mbili baada ya kifo cha Russell, baraza la waelekezi lilikutana na kuchagua A. N. Pierson kuwa mshiriki. Washiriki saba wa baraza wakati huo walikuwa A. I. Ritchie, W. E. Van Amburgh, H. C. Rockwell, J. D. Wright, I. F. Hoskins, A. N. Pierson, na J. F. Rutherford. Kisha baraza hilo la washiriki saba likachagua Halmashauri ya Utekelezi ya watu watatu.