Maelezo ya Chini
d Kwenye mkutano wa kila mwaka uliofanywa katika Januari 5, 1918, wale saba waliopokea idadi ya juu zaidi ya kura walikuwa J. F. Rutherford, C. H. Anderson, W. E. Van Amburgh, A. H. Macmillan, W. E. Spill, J. A. Bohnet, na G. H. Fisher. Kutoka washiriki hao saba wa baraza la waelekezi, wale maofisa watatu walichaguliwa—J. F. Rutherford akiwa msimamizi, C. H. Anderson akiwa makamu wa msimamizi, na W. E. Van Amburgh akiwa mwandishi-mweka-hazina.