Maelezo ya Chini
a Kutoka 1894 hadi 1927, wasemaji wasafirio waliopelekwa na Sosaiti walijulikana kwanza kuwa wawakilishi wa Tower Tract Society, kisha kuwa mapilgrimu. Kutoka 1928 hadi 1936, kukiwa na mkazo ulioongezeka juu ya utumishi wa shambani, waliitwa waelekezi wa utumishi wa kimkoa. Kuanzia na Julai 1936, ili kukazia uhusiano wao ufaao na ndugu wenyeji, wakaja kujulikana kuwa watumishi wa kimkoa. Kutoka 1938 hadi 1941, watumishi wa kanda (eneo) ya dunia walipewa migawo kufanya kazi pamoja na idadi ndogo ya makutaniko kwa njia ya mzunguko, na hivyo kurudi kwenye vikundi vilevile kwa vipindi vya ukawaida. Baada ya kukatizwa kwa kama mwaka mmoja, utumishi huo ulianzishwa upya katika 1942 kukiwa na watumishi kwa akina ndugu. Katika 1948 maneno mtumishi wa mzunguko yalianza kutumiwa; sasa, mwangalizi wa mzunguko.
Kutoka 1938 kufika 1941, watumishi wa kimkoa, wakiwa na daraka jipya, walitumikia makusanyiko ya mahali kwa ukawaida, ambapo Mashahidi kutoka kanda ndogo ya dunia walikutana kwa ajili ya programu ya pekee. Kazi hiyo ilipoanzishwa upya katika 1946, waangalizi hao wasafirio walijulikana kuwa watumishi wa wilaya; sasa, waangalizi wa wilaya.