Maelezo ya Chini
f Kwa kueneza ufanani zaidi, ilisemwa kwamba kuachwa ukiwa kwa Yerusalemu katika 70 W.K. (miaka 37 baada ya Yesu kukaribishwa akiwa mfalme na wanafunzi wake alipopanda punda kuingia Yerusalemu) kungeweza kuelekezea mwaka 1915 (miaka 37 baada ya 1878) kukiwa tokeo la msukosuko wa kuasi sheria ambao walifikiri Mungu angeruhusu kuwa njia ya kuleta mwisho wa mifumo iliyoko ya ulimwengu. Tarehe hiyo ilitokea katika chapa nyinginezo za baadaye za Studies in the Scriptures. (Ona Buku 2, kurasa 99-101, 171, 221, 232, 246-247; linganisha ile iliyochapwa tena ya 1914 na chapa za mapema, kama vile chapa ya 1902 ya Millennial Dawn.) Ilionekana kwao kwamba hayo yalifaa vema na yale yaliyokuwa yametangazwa kuhusu mwaka 1914 kuwa ukitia alama mwisho wa Nyakati za Mataifa.