Maelezo ya Chini
b Sudden Infant Death Syndrome (SIDS, Ugonjwa wa Kifo cha Ghafula cha Kitoto), ambao kwa kawaida huwapata watoto wachanga wenye umri wa mwezi mmoja hadi sita, ndilo jina linalotumiwa wakati watoto wachanga wenye afya nzuri wanapokufa ghafula bila sababu yoyote yenye kuelezeka. Katika hali nyingine inaaminiwa kwamba uwezekano huo waweza kuepukwa ikiwa mtoto mchanga analazwa chali (kwa mgongo) au upande mmoja lakini si kifudifudi. Hata hivyo, hakuna njia ya kulala itakayozuia kila kisa cha Ugonjwa wa Kifo cha Ghafula cha Kitoto.