Maelezo ya Chini
c Huenda Muumba alitumia njia za asili ili kuinua maji hayo na kuyadumisha huko juu. Maji hayo yalinyesha katika siku za Noa. (Mwanzo 1:6-8; 2 Petro 2:5; 3:5, 6) Tukio hili la kihistoria liliathiri sana wanadamu waliookoka na wazao wao, kama vile wataalamu wa kuchunguza asili ya wanadamu wawezavyo kuthibitisha. Tukio hilo limeonyeshwa katika masimulizi yaliyohifadhiwa na watu duniani pote.