Maelezo ya Chini
b Qurani yasema: “Jina lake ni Masih, Isa [Kristo Yesu], mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera.” (Sura 3:45) Akiwa binadamu, Yesu alikuwa mwana wa Maria. Lakini ni baba yupi aliyemzaa? Qurani yasema: “Hali ya Isa [Yesu] kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam.” (Sura 3:59) Maandiko Matakatifu yasema juu ya Adamu kuwa “mwana wa Mungu.” (Luka 3:23, 38) Wala Adamu wala Yesu hakuwa na baba wa kibinadamu; hakuna mmoja wao aliyezaliwa kutokana na ngono iliyofanywa na mwanamke fulani. Kwa hiyo, Adamu alikuwa mwana wa Mungu, na ndivyo ilivyo na Yesu.