Maelezo ya Chini
a Targumi ya Jonathan ben Uzziel (karne ya kwanza W.K.), iliyotafsiriwa na J. F. Stenning, inasema hivi inapofasiri Isaya 52:13: “Tazama, mtumishi wangu, Yule Mtiwa-Mafuta (au, yule Mesiya), atapata ufanisi.” Hivyo hivyo, Talmudi ya Kibabiloni (karibu karne ya tatu W.K.) inasema hivi: “Yule Mesiya—jina lake nani? . . . [; wale] wa nyumba ya Rabi [husema, Yule mgonjwa], kwa kuwa inasemwa, ‘Hakika yeye amebeba magonjwa yetu.’”—Sanhedrin 98b; Isaya 53:4.