Maelezo ya Chini
a Yehova aliwafanyia watu wake uandalizi wa kujiuza utumwani iwapo walitumbukia katika deni—wakawa hasa wafanya-kazi wa kuajiriwa—ili kulipia madeni yao. (Mambo ya Walawi 25:39-43) Hata hivyo, Sheria ilitaka kwamba watumwa watendewe fadhili. Wale waliotendwa ukatili walipaswa kuachiliwa huru.—Kutoka 21:2, 3, 26, 27; Kumbukumbu la Torati 15:12-15.